Header Ads

ad

Breaking News

Waziri Mavunde aelekeza wanakijiji kupewa leseni kuhalalisha uchimbaji wao

Waziri wa Madini Anthony Mavunde kizungumza na wananchi wa Kata ya Ifumbo wilayani Chunya mkoani Mbeya (hawapo pichani), Jumatatu Aprili 28,2025

Na Mwandihi Wetu, Chunya

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameeleza kuwa,  wananchi wa Kata ya Ifumbo wilayani Chunya watapewa leseni 2 kati ya 14 za uchimbaji madini zinazomilikiwa na Kampuni ya G & I katika Bonde la Mto Zira.

Amesema lengo la kuwapa leseni hilo ni kutaka kutambulika rasmi kama wachimbaji halali ili wafanye shughuli za uchimbaji bila usumbufu ikiwa ni hatua ya utatuzi wa mgogoro baina ya wananchi hao na mwekezaji.

Aliyesema hayo Aprili 28, 2025 wakati akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata na Kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya, ambapo aliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo.

“Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake kushughulikia haya mambo kwa haraka na tuko hapa kwa utekelezaji wa maelekezo yake."

Baada ya kusitisha shughuli za uchimbaji madini katika bonde hilo, mwishoni mwa Desemba 2024 aliunda kamati ya wataalam ya kutathmini athari za mazingira yaliyotokana na shughuli za uchimbaji madini katika Mto Zira.

"Kwa kuwa wananchi wa hapa shughuli zenu zinategemea Mto Zira, nimemwelekeza mwekezaji ili aendelee kudumisha ujirani mwema, tumekubaliana katika leseni 14 anazomiliki, atoe leseni 2 kwa ajili ya wananchi wa Ifumbo na Lupa Market ikiwa ni leseni moja kwa kila kijiji," alisema.

Aliongeza kuwa, atafanya tathmini ya mazingira kabla hajakabidhi kwa serikali ya kijiji, tathmini hiyo ni kwa leseni saba zilizopo Ifumbo, kwani saba zilizopo Lupa Market zilifanyiwa tathmini.

Kampuni ya G & I ihakikishe kuwa mazingira yanarejeshwa kama yalivyokuwa awali, kabla uchimbaji huo haujaanza, iweke mipaka ya leseni zao zinapoishia.

Alisema uchimbaji wa eneo la Ifumbo uendelee kusimama mpaka utaratibu wa kimazingira utakapokamilika.

Kwa leseni zilizopo Kijiji cha Lupa Market, mwekezaji anaweza kuendelea na uchimbaji kwa kuwa, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilifanya tathmini ya mazingira, lakini za Ifumbo zinaendelea kusimama mpaka ukaguzi wa mazingira utakapokamilika baada ya siku 21.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Chilo, alielekeza kazi ya upandaji miti katika eneo hilo lifanywe haraka sambamba na kuzingatia utaratibu wa kufanya shughuli za kibinadamu umbali wa mita 60 kutoka kwenye ukingo wa mto kwa mujibu wa sheria.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo

“Nitoe maelekezo kwa NEMC itoe vibali vya ndani ya siku 21 baada ya wahusika kuomba vibali na kukamilsha utaratibu ili kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao kwa tija na bila kubughudhiwa lakini pia Mameja wa NEMC wa Kanda zote kufuatilia tathmini ya mazingira yote ambako shughuli za uchimbaji madini zinafanyika hapa nchini” alisema Chilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya Chunya, Mbaraka Batenga, Mwenyekiti wa Chama ha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya, Noel Chiwanga na Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka walieleza kuwa, wananchi wa Chunya wamenufaika sana na shughuli za madini katika kipindi cha uongozi wake.

Walisema wananchi wa Kijiji cha Ifumbo wamemshukuru kwa kulipa uzito jambo hilo, kulitatua kwa uharaka na kuwapa mrejesho.

Desemba 30,2024 Waziri Mavunde alitangaza kusitisha shughuli za uchimbaji madini katika bonde la Mto Zira na kuahidi kuunda kamati maalum itakayofanya tathmini ya uharibifu wa mazingira uliotokana na shughuli za uchimbaji madini na baada ya kamati hiyo kukamilisha kazi yake, atawapa mrejesho.

Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka





No comments