Header Ads

ad

Breaking News

Mapepele amkabidhi ofisi Nteghenjwa

John Mapepele (kulia) akimkabidhi ofisi ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii, Nteghenjwa Hossea baada ya kupelekwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI

Na Sixmund Begashe

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Nteghenjwa Hossea amekabidhiwa rasmi ofisi na aliekuwa Mkuu wa Kitengo hicho John Mapepele ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, ili kuendelea kuwatumiaka wananchi kwenye ofisi yake hiyo.

Katika zoezi hilo la kihistoria lililofanyika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Patrick Marcelline alimpongeza  Mapepele kwa utumishi wake mwema kwenye Wizara hiyo na kumtakia kila laheri katika ofisi yake mpya.

Marcelline alimkaribisha Nteghenjwa na kumuahidi ushirikiano wakutosha kwenye utekelezaji wa majukumu yake ndani ya Wizara hiyo inayojishughulisha na Uhifadhi pamoja na Utalii nchini.

Aidha, 
Nteghenjwa ambaye awali alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OR-TAMISEMI, ameushukuru uongozi wa Wizara hiyo kwa kumpokea vizuri na kuahidi utumishi mwema katika kuiongoza vyema timu nzima ya mawasiliano ili kufikia lengo la wizara na taifa kwa ujumla kupitia Maliasili na Utalii.

Mapepele aliushukuru uongozi, maafisa wa Kitengo cha Habari, watumishi wote wa wizara hiyo kwa ushirikiano mzuri waliompatia katika kipindi chote alichohudumu hapo.

No comments