BENKI YA NMB YASHINDA TUZO YA BENKI BORA YA MAENDELEO AFRIKA 2017

BENKI ya NMB PLC imeshinda tuzo
mbili katika sherehe za utoaji wa tuzo wa benki bora duniani
zilizofanyika Jijini London, Uingereza. NMB Imetajwa kwa mara ya kwanza
kuwa ni Benki Bora ya Maendeleo Barani Afrika huku tuzo ya pili ikiwa ni
Benki Bora Tanzania 2017 hii ni mara ya Tano Mfululizo.
Kila Mwaka, Jarida la Euromoney
huandaa hafla ya kuyatambua zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi
za kifedha zikiwemo benki kote duniani kwa kuagalia benki bora na ya
kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takribani 100
duniani kote. Tuzo hii huzitambua taasisi za kifedha duniani kote ambazo
zimepata mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao, kwa kuonyesha
ugunduzi na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.
Jarida ya Euromoney liliandika
kuwa,“NMB siyo benki iliyo hai bali ni benki inayofanya kazi. Maamuzi
makubwa yanafanyika kwenye maeneo ya mtaji, biashara na watu yamekuwa
yanafanyika. Katika maboresho hayo, bado benki imeweza kutoa gawio zuri
kwa wanahisa kuliko taasisi yoyote ya fedha nchini.”
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,
Ineke Bussemaker alisema kuwa ubunifu katika huduma, tekinolojia na
uwekezaji katika fedha za kielektroniki kwa msaada wa mtandao mpana wa
matawi na ATM imechangia kuiboresha benki na kuifanya taasisi bora ya
kifedha nchini.
“Kutatua changamoto za jamii ya
watu wasiotumia huduma za kibenki nchini inachukua uwekezaji, ubunifu
na uwezo wa kuwaleta wadau katika malipo na huduma zingine za kifedha,”
alisema bi Ineke
Bi Ineke alisema “kuwa ushindi
wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na benki Bora
Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania
bali Afrika nzima.”
“Tunatoa shukrani zetu wa
wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio
haya makubwa kwa benk, “ alisema Bi Ineke na kuongeza kuwa NMB
itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku
za mbeleni.
Akizungumza kwenye hafla,
Mhariri wa jarida la euromoney Bwana Clive Horwood alisema “mchuano wa
kupata tuzo mwaka huu ulikuwa wa ushindani sana katika taasisi
zilizoshiriki na hivyo kufanya uamuzi kuwa mgumu sana Benki zilizoshinda
na kujipatia tuzo zetu zimechukua hatua kubwa katika mipango yao ya
kibenki. Mabenki huko miaka ya mbele yatakuwa yanaangalia nini unafanya
na pia nini ambacho hukifanyi. Mwaka huu, benki zilizong’ara zimetafsiri
kwa unaga ubaga ni wapi kwenye nguvu Zaidi na kuzingatia maeneo hayo.”
No comments