Mbio za Mwenge zilivyofanyika wilayani Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba
(kulia), akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Shinyanga, Albert Msovela kwa ajili ya kukimbizwa wilayani humo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad
Amour akijaza mafuta katika gari ikiwa ni katika uzinduzi wa kituo kipya cha
mafuta kata ya Kishapu wakati wa mbio za Mwenge wilayani.

Amour akimtwisha ndoo ya maji mwanachi wa kata ya Maganzo wilayani Kishapu
wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita kuzindua mradi wa maji ya Ziwa Victoria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga (katikati) akicheza na ngoma ya wananchi wa jamii ya
Kitaturu eneo la mapokezi ya Mwenge.

Amour akikagua mojawapo ya mashine za kusaga nafaka katika eneo la mradi kwa
mjasiliamali Mabela Masolwa Mhunze wilayani humo.

Watumishi kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu
kushoto mwanasheria wa wilaya, Wilson Nyamunda na Mweka Hazina wa wilaya, Deus
Ngelanizya wakicheza ngoma wakati wa shamrashamra za mbio za Mwenge.

Mwenyekiti wa halmashauari ya Kishapu, Boniphace
Butondo akicheza ngoma wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kijiji cha Kinampanda.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya
wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.

Amour akikagua banda la wanawake wajasiliamali wilayani Kishapu eneo la mkesha
Maganzo.

Mkimbiza Mwenge kitaifa, Frederick Ndahani
akizungumza katika eneo la mkesha kata ya Maganzo wilayani Kishapu.

Amour akizungumza na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafuta Kishapu.

Robert Hokororo, Kishapu
Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa
kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh.
bilioni 3.7.
Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye
alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa
ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa
mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa
mahindi sh. 244.
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka
katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya
mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh.
bilioni 1.1.
Mradi wa ujenzi wa maji ya bomba kutoka Ziwa
Victoria sh. milioni 755 uliofadhiliwa na shirika la Investing in Children and
their Society (ICS), nyumba za walimu sh. milioni 55.8 uliofadhiliwa na mgodi
wa Mwadui.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iligharamia mradi
wa pikipiki kwa vijana wajasiliamali wenye thamani y ash. Milioni 21, hudni
zenye thamani y ash. Milioni 10.5 kwa wanawake wajasiliamali na utengenezaji
bidhaa za ngozi wa Badimi sh. milioni 20.
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Kiongozi wa mbio
za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour aliwataka Watanzania bila kujali
tofauti zao kuuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kulinda
rasilimali zilizopo nchini.
Alisema taifa litaongozwa kwa kufanya kazi kwa
bidii ili tufikie malengo na maendeleo huku akiongeza kuwa tumezunguzkwa na
mito na ardhi yenye rutuba ya hivyo wananchi wajitume.
Alipongeza wilaya kwa kuhakikisha inakuwa na
viwanda huku akiwataka wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa wilayani badala
yake kuwa tegemezi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.
Amour aliasa miradi inayozinduliwa na Mwenge
iwaguse wananchi na waisimamie ili kuleta tija na ufanisi huku akipongeza pia
kwa mapambano dhidi ya Ukimwi na rushwa.
No comments