HALMASHAURI YA CHALINZE YAANZA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Mwamvua Mwinyi, Chalinze
HALMASHAURI
ya Chalinze ,wilayani Bagamoyo,imeanza kuboresha miundombinu ya
barabara zilizoharibika vibaya wakati wa mvua kupitia fedha kutoka kwa
wakala wa barabara (TANROADS)mkoani Pwani.
Aidha halmashauri imesema inajenga vyumba vya madarasa 60 katika shule mbalimbali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya Chalinze ,Saidi Zikatimu ,alisema kiasi cha sh
.mil.140 tayari kimetengwa kwa ajili ya kujenga barabara kutoka Vigwaza
-Buyuni-Kidogozero yenye km .9.4 ambayo mawasiliano yake yamekatika.
“Barabara
hii imeharibika sana ,imekata mawasiliano ,kwahiyo tunashukuru mvua
zimekatika na kilichobakia ni kukarabati na kuboresha maeneo korofi yote
ili kurahisisha usafiri na kuwaondolea adha wananchi ” alisisitiza
Zikatimu .
Alisema katika awamu ya kwanza
wametenga pia sh .mil.131.979.1 na kandarasi ameshapatikana ambae
atatengeneza barabara ya Kikalo-Kwaikonje -Gongo hadi Matipwili .
Barabara nyingine zikatakazotumika kwenye fedha hiyo ni Mkange-Gongo,Kwaruhombo-Kwamdu ma na Kibaoni hadi Kifureta .
Zikatimu alibainisha barabara za
Lugoba -Talawanda ,Magurumatari-Talawanda ,Msata -Pongwe ,Magurumatari
-Talawanda na Pingo-Kidogozero imetengwa mil.167 kwa ajili ya kuboresha
barabara na makalavati .
Mwenyekiti huyo ,alitaja barabara
nyingine iliyotengewa fedha ni Mboga-Diozile,Mdaula-Matuli na Lugoba-
Moreto ambapo itatumika sh.mil.105 ./#.
Hata hivyo ,halmashauri hiyo
imeshatumia mapato yake ya ndani kiasi cha sh.mil.150 kwa kujenga
kalavati na barabara kutoka Kimange-Pongwe Kiona .
Katika kukabiliana na upungufu wa
vyumba vya madarasa ,Zikatimu alibainisha kwamba ,wameshaanza
kushirikiana na wananchi kujenga madarasa katika maeneo mbalimbali
Chalinze .
Alisema hadi sasa vyumba hivyo vipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.
Alielezea kuwa ,kati ya vyumba hivyo Bwilingu wanajenga vyumba 16 kwa nguvu za wananchi lakini halmashauri imechangia mil.21 .
Magome wanajenga vyumba hivyo vitatu na halmashauri imewashika mkono kwa kuchangia mil.saba .
“Tumejipanga kuondoa uhaba wa madarasa ambao bado upo katika shule za msingi na sekondari” alieleza Zikatimu .
No comments