Mesi mdogo wa Simba alamba mkataba Coastal Union
Kulia
ni winga mpya wa Coastal Union Ibrahim Twaha ” Messi” akisaini mkataba
wa miaka miwili wa kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim
El Siagi kushoto ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai.
Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim.
……………………………………
Mwandishi Wetu
TIMU
ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili
kujiimarisha vilivyo katika safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa
kuingia mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili
aliyekuwa winga wa kulia wa Simba,Ibrahim Twaha “Messi”
Utiliaji
saini wa mkataba huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo
mjini hapa na kushuhudiwa na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu
Kassim El Siagi na Meneja wa timu hiyo,Akida Machai.
Akiuzngumza
mara baada ya kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal
Union,Kassim El Siagi alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo
kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .
Alisema
kuwa winga huyo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji
wengine ambao wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa
maendeleo timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu
ujao.
“Niseme tu safari hii tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye
michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha
tunarudisha kombe mkoani hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El
Siagi.
Kwa
upande wake,Ibrahim Twaha “Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo
alihaidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine
katika safari za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Sasa ni kama nimerudi nyumbani kwa sababu awali nilikuwa naitumikia
timu hii hivyo najisikia faraja kubwa kurudi tena Coastal Union mi
nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la kuipa mafanikio “Alisema Messi.
Awali
akizungumza,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu
timu hiyo imedhamiri kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa
ubingwa na kurudisha makali yao ya miaka ya nyuma.
No comments