Mama Salma Kikwete atembelea Hospitali ya Wanawake na Watoto ya Centenary mjini Canberra, Australia
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika plasta ngumu (POP)
kwenye mguu na kumpa pole na kumtakia apone haraka binti Addison
Stephen,6, aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa
hospitalini hapo huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen Miles
(aliyesimama kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali hiyo Mama Elizabeth Chatham.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri
wa siku moja aliyezaliwa na uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali
ya Caniberra nchini Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34,
na Bibi Tania Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi jarida linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto ya Caniberra nchini Australia mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbaali za kutolea huduma hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali wa Australia Mama Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na Gavana Generali wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe 28.7.2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu
ya Australia huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana
Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe wakishuhudia. (Picha zote na John
Lukuwi)
Mwandishi wetu – Canberra, Australia
WAFANYAKAZI
wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya mjini Canberra
wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke
wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya
kina mama wajawazito na watoto.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake,
vijana na watoto wa Hospitali hiyo Liz Chatham wakati akiongea na Mhe.
Mama Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Hospitali hiyo.
Liz alimshukuru
Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) kwa kutembelea Hospitali hiyo na kujioneka kazi wanazozifanya pia
alimpongeza kwa juhudi zake anazozifanya za kuhakikisha wanawake na
watoto wa Tanzania wanapata huduma bora ya afya.
Mkurugenzi
huyo alisema katika Hospitali hiyo wafanyakazi wengi wa sekta ya afya
wanapenda kwenda kufanya kazi Tanzania ili waweze kutoa huduma ya afya
kwa ajili ya mama na mtoto pamoja na watu wengine na kubadilishana
ujuzi wa kazi na wenzao.
Kwa
upande wake Mhe. Mama Kikwete alisema ni jambo la kufurahisha kuona
katika Hospitali hiyo wanawake wenye afya njema wanajifungua katika
mazingira mazuri na watoto ambao ni wagonjwa wanapewa matibabu
na uangalizi wa hali ya juu.
“Nawapongeza
kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia kinamama wajawazito na
watoto, kujifungua iwe sababu ya kuwa na furaha na kusherehekea lakini
siyo tofauti na hapo, nasema hivi kutokana na mazingira halisi ya kule
ninakotoka”.
Pamoja
na kuwa jitihada za makusudi zinafanywa na Serikali bado wanawake na
watoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu
zinazoweza kuzuilika”, alisema Mama Kikwete.
Akiwa
katika Hospitali hiyo Mama Kikwete alipata nafasi ya kuongea na watoto
ambao ni wagonjwa ambao kwa wakati huo walikuwa darasani wanasoma na
aliwaona na kuwajulia hali wazazi waliojifungua Hospitalini hapo.
Utaratibu
wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary mtoto akiwa amelazwa
kipindi ambacho shule hazijafungwa anafundishwa masomo ambayo wenzake
wanafundishwa darasani kwani Hospitalini hapo kuna madarasa na walimu
wanaofundisha watoto wagonjwa.
Mama Kikwete ameambatana na mumewe, Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Australia kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.
No comments