General Motors imerudi tena katika soko la Tanzania ikiwa imeongeza ufanisi zaidi

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa
Kampuni ya QAM Bw, Yusuf Manji, Hiroyuta Kubota kutoka Ubalozi wa Japan
Nchini Tanzania, Toru Nakata Ofisa Mtendaji Mkuu Kutoka Isuzu na Mario
Spangeberg Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa GM Africa kutoka Afrika Kusini
wakikata utepe kuzindua Show Room kubwa na kuuza magari ya Isuzu na
Chevrolet na bidhaa zake hapa nchini katika uzinduzi uliofanyika kwenye
jengo la Quality Group Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam jana.

Viongozi hao wakiangalia ngoma za utamaduzi zilizokuwa zikitumbuizwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya magari yakionyeshwa katika Show Room hiyo.

Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
………………………………………………………………………………..
Wenya magari Tanzania leo wana
sababu ya kutabasamu maana Kampuni ya magari ya General Motors East
Africa (GMEA) Limited wamesaini makubaliano ya kibiashara na Quality
Automotive Mechanization Limited (QAML) ambayo itashuhudia kampuni ya
magari ikiingia kwenye soko la Tanzania.
Kupitia uuzaji mpya, wateja wa
General Motors wataweza kununua bidhaa mpya aina ya Isuzu na Chevrolet
kutoka katika sehemu za mauzo huku wakipata huduma za kimataifa kutoka
katika eneo maalumu la magari hayo.
Akizungumza hi leo wakati wa
sherehe ya kutia saini makubaliano ya biashara, Mwenyekiti wa Kampuni
ya QAM Bw, Yusuf Manji aliahidi wateja ngazi bora ya urahisi na faraja .
“Tumeweka uwekezaji mkubwa na
muhimu kuhakikisha mafanikio ya kituo hiki na kuwezesha kupenya kwa
haraka kwa bidhaa za Isuzu na Chevrolet katika soko hili lenye ushindani
mkubwa”. Alisema
Eneo la mauzo ya magari
limetengenezwa ili kutoa na kuwapatia wateja uzoefu na uimara kwa ujumla
na bidhaa za General Motors, pamoja na kutoa huduma za mauzo na vifaa
vya magari.
Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Bi.
Rita Kavashe alisema Kampuni ya General motors kuingia katika soko la
Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu katika kampuni hiyo
ili kuimarisha uwepo wake katika Afrika Mashariki.
“Tanzania imejitokeza katika soko
na kama General Motors tulitaka kuwa sehemu ya ukuaji huu. Sehemu hii
ya mauzo itakuwa ni hatua ya kuingia kwa bidhaa zetu zenye ubora na
zimetumia utaalamu mkubwa katika utengenezwaji wake ambapo tunatanua
wigo wetu katika ukanda huu. Kupitia uuzaji huu, wateja wetu watanunua
aina mpya za Chevrolet na Isuzu huku wakipata huduma bora”.Alisema
Bi. Kavashe alisema kuingia ndani
ya soko la Tanzania imetokana na kukua kwa kasi kwa biashara ndani ya
ukanda wa Afrika Mashariki hasa katika kuendeleza ushirikiano wa masoko
ya umoja. Soko la jumuia ya Afrika Mashariki lina takribani watu milioni
140 .
“Tanzania ni soko linalokua kwa
kiwango kikubwa na imekua ni soko muhimu tunalolitazamia tunapotafuta
kujikita katika soko lenye watu wengi na idadi inayokua kila kukicha.
Ukuaji wa viwanda na
kuongezeka kwa kipato ili
kutengeneza ongezeko la watu wa tabaka la kati katika nchi hii ina maana
kuwa kuna soko changa la bidhaa zetu, “aliongezea Kavashe.
No comments