Header Ads

ad

Breaking News

JK atoa zawadi ya Idd

Rais Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya Edd el Fitri kwa makundi yenye mahitaji maalum wakiwemo wazee na wenye ulemavu katika mikoa mbalimbali nchini.

Zawadi hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Wizara ya Afya  kwa niaba ya rais, ikisimamiwa na Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Ikulu, Beatrice Fungamo, yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 7.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa viongozi wa vituo mbalimbali vya watu wenye mahitaji maalumu, Fungamo alisema zawadi hizo zimekuwa zikitolewa kwa ajili ya kusaidia makundi hayo katika kusherehekea sikukuu hiyo.

Alisema zawadi hizo hutolewa katika vituo vya kulelea watoto yatima, wasiojiweza, vijana, walemavu na wazee vilivyoko katika mikoa mbalimbali nchini. Msaada huo umetolewa kupitia Wizara ya Afya kutokana na wizara hiyo kuwa na jukumu la kusaidia watu wa aina hiyo.

Fungamo alitaja zawadi hizo mchele, mafuta na mbuzi ambazo zilitolewa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pemba na Unguja kwa upande wa Zanzibar.

"Zawadi hizi zimetolewa kulingana na idadi ya watu waliokuwa katika kila kituo, katika kituo chenye idadi kubwa wanapatiwa kulingana na uhitaji wao," alisema.

Alitaja baadhi ya vituo hivyo ni  Fungafunga kilichopo Morogoro, Tanga mjini, Mabaoni, Chakechake, Shule ya Maadirisho Irambo, Mahabusi ya watoto Arusha mjini na kituo cha Help 2 Kinondoni.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii katika kituo cha Nunge kilichopo Kigamboni, Veronika Msanjira chenye vijana, wazee na watoto yatima 127, alishukuru kwa msaada huo na kuwataka watu mbalimbali wenye uwezo kutoa misaada kwa makundi hayo.

No comments