Banza Stone ametutoa, pengo katika muziki
Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, Ramadhani Masanja 'Banza Stone', amefariki
dunia.
![]() |
Ramadhan Masanja 'Banza Stone' |
Mwanamuziki huyo aliyetamba akiwa na bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' na Tanzania One Theatre (TOT), alikuwa
amelazwa hospitalini kwa muda mrefu.
Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amethibitisha kifo cha Banza
Stone baada ya kupigiwa simu.
“Ni kweli Banza amefariki leo saa saba, tumepata taarifa hizo za msiba, tunasikitika sana kwani alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya muziki,” alisema Asha Baraka.
No comments