Kampuni ya Push Mobile Media yazindua huduma ya kurahisha mawasiliano
Na Mwandishi wetu
Kampuni inayoongoza kwa
huduma ya teknolojia ya mawasiliano, Push Mobile Media imezindua huduma ya
ujumbe kwa njia ya mtandao wa internet ijulikanyo kwa jina la “Bulk Messaging”
kwa lengo la kumwenzesha mtumiaji kufikisha ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika
muda muafaka.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie
Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kufikisha ujumbe muhimu kwa
gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali na kwa mtu binafsi.
Manento alisema kuwa
lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na sekta
nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na kujitangaza.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo kuhusiana na huduma ya
‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma hiyo itamwezesha mtumiaji
kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
“Kama ni
mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa muhimu
utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo ya biashara
zao,” alisema Manento.
“Ili kupata huduma
hiyo, unatakiwa kujiunga kupitia mtandao wetu, www.pushgw.com na kufungua akaunti yako,” alisema Manento.
Alisema kuwa makampuni
au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa wafanyakazi, wateja wao
kuhusiana na biashara na taarifa nyingine.
Mkuu wa Mauzo na Masoko
wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi (Kulia) akielezea
umuhimu wa huduma ya “online bulk Messaging’ kwa sekta
mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ufundi.
“Kwa watu binafsi, unaweza
kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na harusi
na hata kwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la
kuwasiliana na wahariri wao kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,”
alisema.
Mkuu wa Idara ya Mauzo
na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi alisema kuwa huduma hiyo
ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe kwa kiasi cha sh 16 kwa
kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.
Mkuu wa Idara ya Ufundi
wa Kampuni ya Push Mobile Media Daniel
Buchafwe akielezea jinsi ya huduma ya
“online bulk messaging” inavyofanyakazi. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na
Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi.
Alisema kuwa kwa upande
wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na madaktari kuwakumbusha
wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu.
“Unachotakiwa kufanya
ni kujiunga na huduma hii kwa njia ya
mtandao na kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa
na kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.
No comments