Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika (Misa) yampata 'tano' Jokate
Mwandishi wetu
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, (MISA)
imemtangaza mrembo mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo, kuwa
miongoni mwa wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii kwa ukanda wa
nchi za Kusini mwa Afrika ijulikanayo kwa jina la “Misa’s Women to Watch’.
Kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa na MISA wakati wa siku ya
wanawake Duniani, Jokate ambaye ni mfanyabiashara, mwanamitindo, mtangazaji,
mwanamuziki, mbunifu wa mavazi na muigizaji wa filamu amepata nmafasi hiyo
kutokana na juhudi zake katika kuelimisha jamii na hasa afya ya watoto na
kuwawezesha wanawake.
Jokate Mwegelo akikabidhi moja ya bidhaa zake za Kidoti kwa ajili ya kusaidia jamii. Miss Tanzanai namba mbili mwaka 2006 ametangazwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, (MISA) kuwa miongoni mwa wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii.
Taarifa hiyo imesema kuwa Jokate ambaye kwa sasa ana miaka
24, ameweza kuweka msukumo mkubwa katika
jamii mbali ya kujihusisha katika masuala ya ujasiliamali kupitia nembo yake ya
Kidoti.
“Ni mfano wa wanawake walioamua kujiajiri pamoja na kuwa na
elimu ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika masuala ya Siasa, kwa umri wake
mdogo, ameweza kujihusisha na masuala ya afya ya mama na watoto na masuala ya
elimu,” ilisema taarifa hiyo.
Akizungumzia hatua hiyo ya kutambulika, Jokate alisema kuwa
utambuzi wake kutoka Misa ni faraja kubwa na amepata amasa kubwa ya kuendelea
na harakati zake katika elimu, biashara, afya na kuwawezesha watoto wa kike.

Jokate katika pozi
“Nimeamua kuitumikia jamii kutokana na vipaji vyangu,
nashukuru kuona taasisi kama Misa inanitambua na kuniweka katika kundi la
wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii, hii inaonipa taswira kuwa
kile ninachokifanya kinajulikana na ndiyo lengo langu katika jamii,” alisema
Jokate.
Alifafanunua kwa kusema kuwa taarifa hiyo imempa changamoto
na kuwa mbunifu zaidi wa nini cha kufanya katika maisha ya kila siku na hasa
katika kujikwamua kimaisha yeye binafsi na kwa jamii nzima.
Jokate katika pozi
Mbali ya Jokate, orodha hiyo pia imemtaja Miss Tanzania 2013/14
Happiness Watimanywa kutokana na mkakati wake katika masuala ya jamii, Teresa
Chirwa Ndanga (Mwandishi wa habari za uchunguzi Malawi), Josephine Chinele,(Mwandishi,
Malawi), Nashilongo Gervasius (Mwandishi, Namibia), Oshosheni Hiveluah (Mtengenezaji
filamu, Namibia), Mary Pais Da Silva (Mwanasheria
wa Haki za Binadamu Swaziland), Noxolo
Nkabinde (Mwandishi , Swaziland) na Judith Mulenga mwanaharakati wa haki za
watoto nchini Zambia.
No comments