Header Ads

ad

Breaking News

Yanga kuchaguana Juni 15


Kikosi cha Yanga
Na Mwandishi Wetu

UONGOZI wa klabu ya Yanga leo, umetangaza tarehe ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Juni 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, amesema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Aprili 10, mwaka huu katika makao makuu ya klabu hiyo, kimepanga tarehe ya uchaguzi huo utakaowaweka viongozi wapya madarakani.

Kizuguto katika taarifa yake amesema kuwa, kamati hiyo ilipanga kuwa, uchaguzi huo ufanyike Juni 15, hivyo wanachama wenye sifa wajiandae.

Amesema utaratibu wa uchaguzi huo utatangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Alex Mgongolwa.

Kwasasa, klabu hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Yusuph Manji, ambaye tayari ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo.

Manji alitangaza kutogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi ujao, wakati wa Mkutano Mkuu uliofanyika Februari mwaka huu.

No comments