Header Ads

ad

Breaking News

Chezeni mpira, msisikilize kelele

Frank Balile
Na Mwandishi Wetu

MANENO mengi yameanza kusika wakati huu Ligi Kuu Tanzania bara ikielekea ukingo, yapo yanayosema timu zinazowania ubingwa, sasa zimeanza kumwaga fedha kwa wapinzani wao ambao watakutana nao katika mechi za mbele.

Yapo maneno yaliyozaa hivi sasa hata kwenye mitandao ya kijamii kuwa, moja ya klabu hizo zimemjengea nyumba Kocha wa Mbeya City ambao itashuka uwanjani kuumana na Azam FC, mchezo ambao ni muhimu kwa wana lamba lamba ambao wanaongoza ligi.

Maneno hayo ni njia ya kutaka kuidhoofisha Mbeya City ambayo tangu mwanzo wa msimu imeonesha uwezo mkubwa, hata kuzisumbua timu kubwa za ligi kuu Bara na kufanikiwa kuwa katika nafasi ya tatu kimsimamo.

Kikubwa, watanzania wapenda soka walitakiwa kuiunga mkono timu hiyo ambayo kwanza ni changa kabisa, kwa juhudi zake, lakini si kuizushia mambo yanayoichafua na kuiharibia sifa yake nzuri waliyoanza nayo katika ligi hiyo.

Nikiangalia kwa undani tuhuma hizi, naona kama propaganda za watu wengine ambazo lengo lake ni kuidhoofisha Mbeya City ili isifanye vizuri katika mchezo wake dhidi ya Azam FC.

Ukweli, kauli za mitaani na hata kwenye mitandao ya kijamii kwamba, kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi na klabu yenyewe, kwa pamoja watapewa nyuma na basi litakalokuwa likitumiwa na klabu hiyo inayomilikiwa na Jiji la Mbeya.

Mbali na tuhuma hizo kwa makocha hao, pia hata wachezaji walijumuishwa katika kupokea rushwa, kwani wao wanadaiwa kupewa posho ili wacheze chini ya kiwango katika mchezo wa jana.

Watanzania tunachotakiwa kukifanya kwa sasa tunapoelekea mwishoni mwa ligi Bara, ni kuziunga mkono timu zote zinazowania ama zinazopigania kushuka daraja ili zicheze vizuri katika mechi zao zilizobaki.

Kufungwa, kushinda ama sare katika mechi zilizobaki, ni moja ya mchezo, hivyo viongozi na mashabiki wawe tayari kupokea matokeo ya aina yoyote na wala wasiiingize mambo mengine yatakayowachafua wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la timu husika.

Kauli hizo si kwa Mbeya City, ni kwa timu zote ambazo ambazo ziko kwenye Ligi Kuu Bara, hasa wakati huu wa kuelekea mwishoni mwa ligi hiyo ambayo imebakiza michezo isiyozidi miwili.

Pia, lazima watu wajiulize, hivi kama timu ina uwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote, kwanini ishindwe kuwa na timu imara na ya ushindaji haha kutegemea kutafuta wachezaji wa timu pinzani na kuwarubuni ili wapate matokeo mazuri?

Hizo propaganda zinatakiwa kufanyiwa kazi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Bodi ya Ligi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kubaini kama kweli kocha huyo kajengewa nyumba, wachezaji kuhongwa na hata uongozi kuahidi basi la kusafiria.

Hatua hiyo itakuwa ya kujiridhisha kwa vyombo hivyo, ili kuondoa maneno yanayozidi kuzagaa mitaani, ambayo yanaweza kuchochea hali ya hatari hasa pale timu itakapofungwa katika mchezo huo.

Mashabiki wao watapeleka mawazo yao katika uvumi huo, hata kama walikwenda uwanjani na kushuhudia mchezo husika, hivyo mashabiki wa soka tuache kuvumisha maneno yanayoweza kusababisha vurugu  waliotajwa.

Kwanza, uvumi huo tayari umewavuruga kisaikolojia kuanzia kocha huyo ambaye kwa msimu huu tunaweza kusema ni kocha bora, wachezaji wake na hata viongozi wa klabu hiyo inayomilikiwa na Jiji la Mbeya.

Staa Spoti tunaamini, wale wote wanaozusha mambo hayo, wataacha kwani yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani miongoni mwa viongozi, wachezaji na hata benchi la ufundi.

Tunaamini kwamba, Azam FC imejiandaa kwa muda mrefu kushiriki ligi hiyo, hata katika misimu miwili imeweza kushika nafasi ya pili kimsimamo na kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa, hivyo lolote linaweza kutokea katika mchezo huo.

Kikubwa ni kwamba, waamuzi watakaopangwa katika mechi zilizosalia, wahakikishe wanachezesha kwa kufuata sheria 17 za mpira wa miguu ili nchi ipate mwakilishi sahihi katika michuano ya kimataifa.

Tunazitakia mechi nzuri 'fare play' zilizobaki, timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo ambayom inaelekea ukingoni.

0713 405652

No comments