Gerrard apiga bao la 100, wakitoka sare na Newcastle
![]() |
Steven Gerrard |
NAHODHA wa timu ya Liverpool, Steven Gerrard, amefikisha mabao 100 ya kufunga
akiitumikia timu yake katika mechi za Ligi Kuu England, baada ya kufunga bao katika mchezo
wa leo dhidi ya Newcastle United uliomalizika kwa mabao 2-2.
Gerrard mwenye 33, aliyeifungia England bao katika mechi waliyoibuka na ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Poland kwenye Uwanja wa Wembley, Jumanne iliyopita, mechi ya kuwania
kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Ameifungia Liverpool bao la mkwaju wa penalti leo, baada ya beki wa Newcastle, Mapou
Yanga-Mbiwa kuchezea vibaya Luis Suarez na kutolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Gerrard alifunga mkwaju wa penalti dakika ya 42 na Sturridge dakika 72, wakati mabao ya
wapinzani wao yalifungwa na Cabaye dakika ya 23 na Dummett dakika ya 56.
No comments