Header Ads

ad

Breaking News

Chelsea yaipasua Cardiff 4-1, Arsenal kiboko

 
 LONDON, England
CHELESEA, leo imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1, dhidi ya Cardiff, katika mechi ya

Ligi Kuu England iliyopgwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London.

Cardiff ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Mutch dakika ya 10, lakini furaha yao
ilizimwa na Hazard dakika ya 33, kabla ya Samuel Eto'o kuiongezea bao la pili dakika ya 66.

Bao hilo ni la kwanza kwa mshambuliaji huyo aliyejiunga na klabu hiyo majira ya kiangazi
akitokea Urusi.

Chelsea ilijipatia bao la tatu dakika ya 78, lilifungwa na Oscar, kabla ya Hazard kumalizia bao

la nne dakika ya 78.

Kwa ushindi huo, Chelsea wamefikisha pointi 17, wakiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Arsenal wenye pointi 19, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Norwich.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Wilshere dakika ya 18, Ozil dakika ya 58 na 88 na Ramsey dakika ya 83, wakati wapinzani wao walipata bao lao dakika ya 70 likiwekwa wavuni na Howson.

No comments