Vitz mbili kushindaniwa fainali ya Fiesta
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Push Media Mobile itatoa magari mawili aina ya Vitz kwa mashabikli wa tamasha la Fiesta lililopangwa kufanyika Jumamosi ijayo kwenye viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Masoko na Mauzo wa Push Media Mobile, Rugambo Rodney, alisema magari hayo mawili yana thamani ya sh. milion 17 na ili kushinda, mshindani anatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 na pia zawadi nyingine kama fedha taslimu kiasi cha sh. 100,000 kwa kila siku.
Rodney alisema kuwa, wameamua kutoa zawadi ya magari hayo kutokana na kuthamini mchango wa mashabiki wa muziki na jamii katika sekta ya burudani na michezo.
Alisema kuwa, zawadi ya magari hayo itahitimisha jumla ya magari manne waliyotoa mwaka huu katika tamasha la Fiesta.
"Gari la kwanza lilitolewa Kigoma na la pili mkoani Mwanza, pia tumetoa pikipiki na fedha taslimu kibao kwa mashabiki mbalimbali mikoani ambako Fiesta ilifanyika, tunawaomba mashabiki wajaribu bahati yao, kwani nafasi ya kushinda ni kubwa," alisema Rodney.
Kwa mujibu wa Rodney, shindano hilo linafanyika mikoa yote, hivyo nafasi ya kushinda ni kubwa. Mwaka jana, kampuni hiyo ilitoa magari mawili katika tamasha la Fiesta.
![]() |
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Media Mobile, Rugambo Rodney |

No comments