Header Ads

ad

Breaking News

UWAKILISHI KWENYE MKUTANO MKUU TFF

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imesema uwakilishi wa ujumbe kwenye Mkutano Mkuu
unaanzia kwenye chama cha mpira wa miguu cha mkoa, kufuatiwa na chama
shiriki na baadaye klabu ya Ligi Kuu.

Mwongozo huo juu ya uwakilishi wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu
umetolewa kutokana na maombi ya Sekretarieti ya TFF kwa kamati hiyo
iliyokutana jana (Septemba 16 mwaka huu) baada ya kubaini baadhi ya
wajumbe wanashikilia nafasi mbili kwenye vyama tofauti.

Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kuna makundi ya aina tatu ya wanachama
wanaounda TFF. Makundi hayo ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za
Ligi Kuu.

Sekretarieti ya TFF imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wa
mikoa ambao pia ni viongozi wa vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, hivyo wana
nafasi zaidi ya moja ya kuingia kwenye Mkutano Mkuu.

Hivyo, kutokana na mwongozo huo ushiriki wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu
wa TFF utaanzia chama cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye
klabu za Ligi Kuu.

Pia nafasi ambazo zinaweza kuwakilishwa kwenye Mkutano Mkuu kama
mhusika hayupo ni za Mwenyekiti atakayewakilishwa na Makamu Mwenyekiti,
na Katibu atakayewakilishwa na Katibu Msaidizi.  Nafasi za ujumbe wa
Mkutano Mkuu na ile ya mwakilishi wa klabu hazina uwakilishi kama mhusika
hayupo.

No comments