Header Ads

ad

Breaking News

KAYUNI KUHUDHURIA KOZI YA WAKUFUNZI WA CAF

Sunday Kayuni
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Sunday Kayuni atashiriki warsha ya wakufunzi wa makocha wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika kuanzia Oktoba 22-24 mwaka huu.

Warsha hiyo iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya wakufunzi wake itafanyika nchini
Cameroon. Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa makocha watahudhuria
warsha hiyo.

Madhumuni ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao, kubadilishana uzoefu.
Pia kuwapa methodolojia mpya ya ufundishaji na muongozo kuhusu mfumo wa
leseni za makocha ambao watautumia katika nchi wanazotoka.

Mbali ya Kayuni Tanzania, wakufunzi wengine ni Ahmed Babiker (Sudan),
Amadou Shaibu (Nigeria), Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu Fred Osam
(Ghana), Edussei Anthony (Ghana), Fathi Nossir (Misri), Faouzy Altaisha
(Sudan) na Fran Hilton Smith (Afrika Kusini).

Wengine ni Francis Oti-Akenteng (Ghana), Honour Janza (Zambia), Kasimawo
Laloko (Nigeria), Mahmoud Saad (Misri), Paul Hamilton (Nigeria), Serame
Letsoaka (Afrika Kusini), Shawky Abdel Shafy (Misri), Thondoo Govinder
(Mauritius) na Ulric Mathiot (Seychelles),

No comments