LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA NNE
![]() |
Kikosi cha Yanga |
inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 18 mwaka huu) kwa mechi saba katika
viwanja saba tofauti.
Vinara wa ligi hiyo, JKT Ruvu wanaonalewa na Kocha Mbwana Makata
watakuwa ugenini Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya
Ruvu Shooting ya Charles Boniface Mkwasa. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa
kivutio kikubwa kwa washabiki mkoani Pwani kutokana na aina ya soka
inayochezwa na timu hizo.
Baada ya sare dhidi ya Mbeya City wikiendi iliyopita, Yanga inaendelea kubaki
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo itacheza na
Tanzania Prisons katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mbelwa
kutoka Pwani.
Nayo Simba itaumana na Mgambo Shooting Stars ya Tanga katika mechi
itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mechi hiyo itakuwa chini ya Kamishna David
Lugenge kutoka Iringa.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Oljoro
JKT kutoka Arusha na wenyeji Kagera Sugar wakati Azam na Ashanti United
zitakwaruzana kwenye uga wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es
Salaam.
Mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara ndiye atakayechezesha mechi kati ya
Coastal Union na Rhino Rangers itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga. Mtibwa Sugar inarejea uwanja wake wa Manungu ulioko Turiani mkoani
Morogoro ambapo inaikaribisha Mbeya City ya Kocha Juma Mwambusi.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea kesho
(Septemba 18 mwaka huu) kwa mechi moja ambapo Lipuli ya Iringa ambayo
wikiendi iliyopita ilicheza Mkamba mkoani Morogoro inapita mjini Morogoro
kuikabili Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.
No comments