Header Ads

ad

Breaking News

MABINGWA ARS KUPONGEZWA DAR

Timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Airtel Raising Stars (ARS) ya
Tanzania imeandaliwa hafla ya kuipongeza kwa kunyakua ubingwa katika
mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.
 
Hafla hiyo ya kuipongeza pamoja na kupata chakula cha mchana itafanyika
leo (Septemba 24 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hoteli ya Kilimanjaro
Kempinski na kuongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
 
Timu hiyo iliyorejea nchini jana (Septemba 23 mwaka huu) usiku katika
mchezo wa fainali ya mashindano hayo iliifunga Kenya. Kwa upande wa
wavulana, timu hiyo ilitolewa na Zambia katika hatua ya nusu fainali.
 
Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka nchi za Burkina Faso, Chad, Congo
Brazzaville, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),
Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia.
 
Kombaini ya timu hizo zilizokuwa chini ya makocha Rogasian Kaijage na
Abel Mtweve iliundwa baada ya mashindano ya Airtel Raising Stars
yaliyohusisha wasichana na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 17 na
kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Septemba mwaka huu.

No comments