Header Ads

ad

Breaking News

TWIGA STARS YAPANGIWA ZAMBIA AWC

Twig
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imepangiwa
kucheza na Zambia katika mechi za kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia.
 
Twiga Stars itaanzia ugenini jijini Lusaka ambapo mechi ya kwanza
itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwakani wakati ile ya marudiano
itafanyika kati ya Februari 28 na Machi 2 mwakani jijini Dar es Salaam.
 
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia, raundi ya pili ambayo ndiyo ya
mwisho itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe. Mechi ya
kwanza itakuwa Dar es Salaam kati ya Mei 23 na 25 mwakani wakati ile ya
marudiano itakuwa kati ya Juni 6 na 8 mwakani.
 
Nchi 25 zimeingia katika mashindano huku mabingwa watetezi Equatorial
Guinea, makamu bingwa Afrika Kusini na Cameroon iliyoshika nafasi ya tatu
katika fainali zilizopita zikiingia moja kwa moja katika raundi ya pili.

No comments