MECHI YA TOTO, POLISI DOM KUPIGWA J2
Mechi namba 12 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Toto Africans na
Polisi Dodoma iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu)
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza imesogezwa mbele kwa siku moja.
Timu hizo za kundi C sasa zitapambana Jumapili (Septemba 29 mwaka huu)
kwenye uwanja huo huo ili kupisha mechi namba 10 kati ya Pamba na Stand
United FC ya Shinyanga itakayochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka
huu).
Mechi nyingine za kundi hilo zitakazochezwa Jumamosi ni Mwadui na Polisi
Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) wakati Kanembwa JKT na
Polisi Mara zitacheza kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

No comments