Header Ads

ad

Breaking News

Man United, Man City, Real Madrid zatesa Ulaya

Cristian Ronaldo
MANCHESTER, England
 
WAYNE Rooney, aliifungia timu yake ya Manchester United mabao mawili

yaliyomwezesha Kocha wake, David Moyes kupata ushindi wa kwanza katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku wakitoka uwanjani na jumla ya
mabao 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Manuel Pellegrini pia alikuwa na nafuraha baada ya kuingoza Manchester City
kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Viktoria Plzen, mabao yaliyofungwa
na Edin Dzeko, Yaya Toure na Sergio Aguero.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich walianza vizuri baada ya
kutoka uwanjani wakiwa na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya CSKA Moscow
chini ya kocha wao mpya Pep Guardiola, wakati Cristiano Ronaldo akiwapeleka
wapinzani wake wavuni mara tatu katika mechi ambayo Real Madrid waliibuka
na ushindi wa mabao 6-1 vdhidi ya Galatasaray, huku Juventus ikibanwa na FC
Copenhagen na kufungana bao 1-1.

Rooney ameingia katika historia ya Manchester United kwa kuifungia mabao,
alifunga mabao mawili katika mechi ya kwanza ya Klabu Bingwa Ulaya na
kuiwezesha timu yake kutoka uwanja wakiwa na mabao 4-2 dhidi ya Bayer
Leverkusen.

Mshambuliaji huyo aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 22, akitumia
vizuri mpira wa krosi uliopigwa na Patrice Evra, Robin Van Persie aliiongezea
bao la pili dakika ya 59, Rooney aliwarudisha tena kati dakika ya
70, kabla ya Antonio Valencia  kumalizia bao la nne dakika ya 79.


Mabao ya wapinzani wao yalifungwa na Simon Rolfes  dakika ya 54 na  
Omer Toprak  dakika ya 88.


Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Viktoria Olzen,
katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Doosan Arena. Bao la kwanza
lilifungwa dakika ya Edin Dzeko  dakika ya 48,  Yaya Toure  aliiongezea bao la
pili dakika ya 53, kabla ya Sergio Aguero  kumalizika bao la tatu dakika ya 58.

Kwa upande wa mabingwa watetezi, Bayern Munich walinza vema kutetea
ubingwa, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya CSKA Moscow,
mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Mabao ya Munich yaliwekwa kimiani na David Alaba dakika ya tatu, Mario
Mandzukic dakika ya 41 na Arjen Robben dakika ya 68.

Real Madrid ilifanya kufuru baada ya kuibamiza Galatasaray mabao 6-1,
ingawa Galatasaray walianza mchezo huo kwa bguvu na kulisakama lango la
wapinzani wao.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Isco  dakika ya 33, Karim Benzema 

dakika ya 54, 81 na Cristiano Ronaldo  dakika ya 63, 66, 90.
 
Gareth Bale alianza katika benchi, lakini aliingia na kutoa pasi nzuri iliyotumia

vizuri na Ronaldo, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Umut Bulut.
Juventus na FC Copenhagen, zilitoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1.

Bao la FC Copenhagen lilifungwa na Nicolai Jorgensen dakika ya 14, wakati
wa JUve liliwekwa kimiani na Fabio Quagliarella  dakika ya 54.

Paris Saint-Germain ilitoka uwanjani na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya
Olympiakos, mabao yalifungwa na Edinson Cavani  dakika ya 19, Thiago Motta
 dakika ya 68, 73 na Marquinhos  86, wakati bao la wapinzani wao lilifungwa na
Vladimir Weiss dakika ya 25.

TImu ya  Benfica, ilikuwa na furaha baada ya kuiliza Anderlecht kwao mabao 2
-0. Mabao ya washindi yalifdungwa na Filip Djuricic na Luisao, wakati Real
Sociedad ilikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk, mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Estadio Municipal de Anoeta, huku mabao yote
yalifungwa na Alex Teixeira dakika ya 65 na 87.

 

No comments