Yanga yaishusha Azam FC, yaichapa JKT Oljoro
![]() |
Yanga |
Na Mwandishi
Wetu, Arusha
BAO pakee
lililofungwa na beki wa Yanga, Mbuyu Twite dhidi ya Oljoro JKT ya mjini hapa leo, limeiwezesha timu yake hiyo kuchupa hadi nafasi ya pili katika msimamo wa
Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kuiporomosha Azam iliyokuwa ikishika nafasi
hiyo kwa muda mrefu sasa.
Matokeo hayo
yameiwezesha Yanga kufikisha pointi 20 kutokana na mechi 10, ikiwa nyuma ya
Simba inayoshikilia usukani kwa kwa pointi zao 22, timu zote hizo zikwia
zimeshuka dimbani mara 10.
Azam
iliyopokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam jana, imebakiwa na pointi zake 18 na sasa inashika nafasi ya tatu katika
ligi hiyo inayojumuisha timu 14.
Katika
mchezo huo wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini hapa,
Yanga iliuanza kwa kasi ya wastani ambapo washambuliaji wake walipata nafasi
kadhaa za kufunga ambazo hata hivyo walishindwa kuzitumia vema.
Kwa upande
wao, JKT Oljoro wanaonolewa na kipa wa zamani wa Yanga, Mbwana Makata,
walionyesha upinzani wa aina yake kwa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati
na kwamba iwapo wangekuwa makini, wangeweza kupata bao la mapema kama
washambuliaji wake wangekuwa makini.
Kwa ujumla,
mchezo huo ulitoa burudani ya nguvu kwa wapenzi wa soka wa jijini hapa
waliojitokeza kwa wingi kuwaona nyota wa Yanga, hasa waliosajiliwa msimu huu.
Miongoni mwa
nyota waliokuwa kivutio uwanjani hapo, ni Twite na Didier Kavumbagu ambapo
mashabiki wa soka wa hapa walionekana kuwasogelea kutaka kuwaona kwa karibu
zaidi.
Katika mechi
nyingine iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, timu ya Ruvu
Shooting, jana ilitumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuichapa Polisi
Morogoro mabao 2-1.
Polisi Moro
walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Malimi Busungu dakika ya 66,
lakini Ruvu Shooting walisawazisha dakika ya Shaban Suza dakika ya 69, kabla ya
Said Dilunga kuihakikisha timu ushindi kwa kuifungia bao la pili dakika ya 77.
No comments