Simba yateswa na mechi za ugenini
![]() |
Kikosi cha Simba |
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
TIMU ya soka ya Polisi Morogoro, jana ilifanikiwa kuibana
Simba, na kutoka nayo sare ya bao 1-1, katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Polisi Moro iliyopo mkiani mwa ligi hiyo, ilianza mchezo huo
kwa kasi na kufanya mashambulizi langoni mwa Simba, lakini safu ya ulinzi ya wapinzani wao
iliyokuwa chini ya Mkenya Pascal Ochieng, ilikuwa imara kuhakikisha nyavu zao
hazitikiswi.
Mashambuliji ya maafande wa Polisi Moro, yalizaa matunda dakika
ya 33, baada ya Mokili Lambos kuifungia timu yake bao.
Lambo aliyetokea kwenye benchi kuchukua nafasi ya John
Bosco, aliukwamisha mpira huo wavuni, baada ya kuubetua kiufundi mpira wa
krosi uliopigwa kutoka upande wa kulia na kumpita kipa Juma Kaseja Juma .
Kufungwa kwa bao hilo kuliwafanya Simba watulie na kucheza
soka zuri la kiufundi, lakini washambuliaji wake, Emanuel Okwi, Felix Sunzu, Mrisho
Khalfan Ngasa na Amri Kiemba, walishindwa kusawazisha bao hilo dakika 45 za
kwanza za mchezo huo.
Simba walikianza kipindi cha pili kwa kulisakama lango la
Polisi, huku wakionana vizuri na kuwachanganya mabeki wa wapinzani wao, kabla
ya mpira wa kona uliopigwa na Emmanuel Okwi ulitua kwa Amri Kieemba ambaye
hakufanya makosa, kwa kuukwamisha wavuni dakika ya 57.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 23, ikiwa na sawa
na Yanga, ambao jana waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Mgambo JKT,
mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
ciao
No comments