Tanzania Prisons wapata ajali wakielekea kuivaa Magombo Tanga
![]() |
Prisons |
Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI
sita wa timu ya soka ya Tanzania Prisons
ya Mbeya inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jana ilipata ajali
maeneo ya Segera na Hale mkoani Tanga, wakati wakielekea jijini Tanga kucheza
na Mgambo Shooting.
Akizungumza na SuperStar kwa
njia ya simu jana, Kocha mkuu wa timu hiyo, Jumanne Challe, alisema kuwa,
wachezaji 16 waliumia katika ajali hiyo, ambapo sita wamelazwa katika hospitali
ya Muheza.
Aliwataja wachezaji
waliolazwa ni David Mwantika, Lugano Mwagama, David Mwasongwe, Sino Agustino,
Halid Fungambeck na Sadick Jumbe.
“Tulipata ajali mbaya jana
(juzi) maeneo ya Segera na Hale, tukiwa njiani kwenda Tanga, kama si dereva
wetu kukwepa, tungekufa wote, maana tungegongana uso kwa uso, lakini
alifanikiwa kulikwepa na tukapinduka mara tatu.
“Wengine si wazima sana,
wengi wao wameumia mbavu, shingo, magoti, migongo viuno, na hata mimi niliumia
mguu wa kushoto,” alisema Challe.
Kocha huyo alisema kwamba,
daktari wa timu hiyo anaandaa ripoti ya wachezaji, na ikikamilika, wataipeleka
kwa msimamizi wa kituo ili aweze kuiwasilisha katika ofisi za Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
No comments