Simba, Yanga kibaruani kesho
LIGI Kuu Tanzani Bara,
inatarajia kuendelea tena hii kesho, ambapo Mabingwa wa ligi hiyo Simba na Yanga
watashuka dimbani.
Simba watakuwa wenyeji
wa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam, wakati Yanga watakuwa ugenini kucheza na Oljoro
JKT kwenye Uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Masikio ya mashabiki wa
soka hapa Tanzania
yatakuwa kwenye viwanja vyote viwili kutokana na upinzani wa pointi uliopo kwa
timu tatu Simba, Yanga na Azam FC.
Hadi leo, Simba inaongoza
kwa pointi 19 wakiwa wamecheza mechi tisa sawa na Yanga mwenye pointi 17, Azam
ikiwa nafasi ya pili 18 na mchezo mmoja mkononi.
Kutokana na matokeo
hayo kazi kubwa itakuwa kwa Simba na Azam ambao wanakutana kila mmoja akitaka ponti
hizo tatu ili kuweza kusonga mbele.
Yanga tayari wamewasili
jijini Arusha juzi, huku wachezaji wakiwa wenye furaha baada kupewa fedha kwa
ajili ya kuwapa morali katika mchezo wa kesho.
Ili
wawapite wapinzani wao Simba na Azam wanatakiwa kushinda mchezo wa leo huku
wakisikilizia matokeo ya wapinzani wao na siyo kutoa sare.
Huko Msimbazi, nako mambo
siyo shwari kutokana na mpasuko uliopo kati ya viongozi na wachezaji, leo
watakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha wanashinda ili mambo yakae sawa.
Timu ya Simba iliweka
kambi visiwani Zanzibar
kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kesho baada ya kupoteza pointi sita kwa
kutoka sare mara tatu mfululizo.
Azam wao bado wanatakiwa
kushinda na hata kama wakitoka sare bado ana
faida ya mchezo mmoja mkononi.
Mbali na mechi hizo,
African Lyon itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Chamazi huku
Ruvu Shooting ikiikaribisha Polisi Moro Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
No comments