MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO
*Achangisha fedha za ujenzi wa shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini
ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika
Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga,
Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo
na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji
fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya
Vuchama Mosque Islamic Centre, jana Oktoba
26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya
Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo
katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada
hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la
Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko
wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na
Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, jana Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. jana Oktoba 26, 2012. Picha zote na OMR
No comments