MTIBWA SUGAR, JKT RUVU YASOGEZWA MBELE, KUCHEZA NOV 7
Mechi
namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu iliyopangwa
kuchezwa Novemba 3 mwaka huu Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, sasa itafanyika
Novemba 7 mwaka huu.
Mabadiliko
hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi
namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mechi hiyo
awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3 mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa
kwa mechi za Super Week zilizooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni
cha Super Sport cha Afrika Kusini.
No comments