AZAM YASUFUKUZIA USUKANI WA LIGI
![]() |
Azam FC |
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Oktoba 24 mwaka huu) kwa mechi nne za raundi ya tisa huku Azam ikiusaka usukani
wa ligi hiyo ikiwa mwenyeji wa Ruvu Shooting.
Mechi
hiyo namba 60 ambayo kama Azam itashinda itafikisha pointi 20, hivyo kuwa
kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Yanga
itawakaribisha Polisi Morogoro ambao ndiyo wa mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu
ya Vodacom hivi sasa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Alex
Mahagi kutoka Mwanza ndiye atakayepuliza filimbi kwenye mechi hiyo namba 62.
Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba na Michael Mkongwa, wote kutoka Iringa wakati
mwamuzi msaidizi ni Oden Mbaga anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) wa Dar es Salaam.
Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya African Lyon ya Dar
es Salaam ambao ni wageni wa Coastal Union inayonolewa na Hemed Moroco. Nayo
Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko kwenye
mashamba ya miwa Turiani mkoani Morogoro.
No comments