FDL KUANZA KUTIMUA VUMBI OKT 24
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 24 mwaka
huu) kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Kundi
A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza na Mbeya City kwenye
Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Small
Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Nayo
Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi ulioko Mufindi mkoani
Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa (Oktoba 25 mwaka huu)
kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa utakaofanyika Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
Mechi
za kundi B kwa kesho ni Ndanda dhidi ya Transit Camp katika Uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na Moro United kwenye Uwanja wa
Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors v Tessema
(Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United (Uwanja wa Chamazi).
Kundi
C kesho (Oktoba 24 mwaka huu) ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi
Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
No comments