Benzema akubali mambo ya Mourinho
![]() |
Jose Mourinho |
MADRID, Hispania
Karim Benzema amesisitiza kuwa,
ataendelea kuitumikia klabu yake ya Real Madrid inayocheza ligi kuu ya Hispania ‘La
Liga’.
Mshambuliaji huyo kutoka Ufaransa,
amekuwa akihusishwa kuondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari
mwakani, baada ya Real kumtupia macho mshambuliaji wa Atletico Madrid,
Radamel Falcao.
"Kocha ananiamini sana na
tunafanya kazi nzuri kutokana na imani yake kwangu. Na sasa nimeiva katika kila
kitu. Nilikuwa na mambo mengi yakipanda na kushuka tangu nilipotua Madrid, lakini
bado nipo hapa.
"Jose Mourinho, ni bonge la
kocha na anatuunga mkono. Hofu ni sehemu ya maisha yangu tangu nilipokuwa Lyon,
lakini hapa ni zaidi kwani nipo katika klabu bora duniani."
No comments