Messi ni bora anastahili Ballon d'Or- Vilanova
![]() |
Lionel Messi |
BARCELONA, Hispania
KOCHA wa Barcelona,
Tito Vilanova, amezidi kumpa nafasi kubwa Lionel Messi,
kubeba uchezaji bora ‘Ballon d'Or’.
Messi, alifunga mabao matatu ‘hat-trick’,
katika mechi dhidi ya Deportivo La Coruna ya ligi kuu Hispania na kuisaidia timu yake kuibuka na
ushindi mnono.
“Hastahili kwa sababu ya kile
alichokifanya siku iliyopita, lakini anastahili kwa sababu ya yale aliyofanya
kwa mwaka mzima,” alisema Vilanova.
Vilanova aleweka wazi kuwa,
hamfanyii kampeni Messi, lakini ni kwamba, “hakuna mchezaji atakayefanya kile
alichokifanya Messi.”
No comments