AZAM, RUVU SHOOTING BAO 1-1
Na Mwandishi Wetu, Chamazi
TIMU za Azam FC na Ruvu Shootin, leo zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ruvu
Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Seif Abdallah.
hata hivyo, wakiwa bado wana furaha, waliumizwa na mshambuliaji wa kimataifa wa kutoka Ivory Coast, Kipre
Tchetche, bao lililozifanya timu hizo kugawana pointi.
No comments