Man Utd, Barcelona safi Ulaya, Chelsea mambo magumu
![]() |
Manchester United wakishangilia bao |
LONDON, England
RAUNDI ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya iliyoanza Machi mwaka huu, ilihitimishwa jana usiku, huku kukiwa na
matokeo ya kushangaza katika mechi za juzi usiku.
Manchester United ikicheza kwenye
uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford, jijini London, England, ilitoka nyuma
na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Sporting Braga 3-2, shukrani zikienda kwa Javier
Hernandez aliyefunga mara mbili.
Alan aliifungia timu yake ya Ureno
mara mbili kuipa uongozi wa mabao 2-0 hadi dakika ya 20, kabla ya Chicharito
kubadili matokeo kuwa 2-1 dakika tano baadaye na Jonny Evans aliongeza la pili
katika kipindi cha pili.
Mabingwa watetezi wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya, Chelsea, walifungwa mabao 2-1 na Shakhtar Donetsk ya Ukraine
kwenye Uwanja wa Donbass Arena kwa mabao ya Alex Teixeira na Fernandinhola
kabla ya bao la kufutia machozi lililofungwa na Oscar dakika za mwisho.
Mabingwa wa Scotland, Celtic
waliikamata Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp, lakini bao la dakika za mwisho
la Jordi Alba, liliwezesha miamba ya Catalan kupata ushindi wa mabao 2-1 baada
ya Andres Iniesta kusawazisha bao la kuongoza la Giorgios Samaras dakika ya 18.
Kwingineko, Spartak Moscow iliifunga
Benfica mabao 2-1, ikiwa ni baada ya Jardel kujifunga, wakati Juventus ilitoka
sare ya bao 1-1 na Nordsjaelland ya Denmark, wakati Roberto Soldado alifunga
mabao matatu ‘hat-trick’ kuiwezesha Valencia kuichapa BATE Borisov mabao 3-0.
Katika mchezo mwingine, penalti iliyofungwa
na Thomas Muller, iliiwezesha Bayern Munich kuichapa Lille bao 1-0 na CFR Cluj
iliibana Galatasaray na kutoka nayo sare ya bao 1-1 mjini Istanbul, Uturuki.
Matokeo ya mechi za juzi kwa ufupi
KUNDI E
Shakhtar Donetsk
2-1 Chelsea
Nordsjaelland
1-1 Juventus
KUNDI F
BATE Borisov 0-3 Valencia
Lille
0-1 Bayern Munich
KUNDI G
Spartak Moscow
2-1 Benfica
Barcelona
2-1
KUNDI H
Manchester United
3-2 Sporting Braga
Galatasaray
1-1 CFR Cluj-Napoca
No comments