Bolt afanya maajabu, avunja rekodi yake
Usain Bolt akimaliza mshindi wa mita 100 olimpiki.
LONDON, England
"Kuna
watu wengi walisema siwezi kushinda hapa, kulikuwa na mengi pia
yalisemwa. Ni hisia za aina yake kuona nimeyashinda yote hayo na
kuthibitisha kuwa bado mimi ni namba moja na bado mimi ni bora"
BINGWA
mara nne wa Olimpiki, Usain Bolt wa Jamaica, amesema anakaribia kuwa
nguli wa mchezo huo duniani, baada ya Jumapili kutetea vema dhahabu yake
ya fainali za Olimpiki katika mbio za mita 100.
Bolt
(25), alishinda kwa muda wa rekodi akitumia sekunde 9.63 na sasa yu
tayari kufanya tafakuri sahihi za kutetea na medali ya mita 20, jijini
London.
"Dhahabu
hii inamaanisha kuwa niko hatua moja tu kuelekea kuwa nguli wa mchezo
huu, hivyo natakiwa kufanya kazi ngumu na ya ziada kufanikisha hilo,”
alisema na kuongeza: "Kwamba niko hatua moja tu kabla.
"Naelekea kukimbia mita 200 sasa, hivyo napaswa kuangalia mbele kuona namna navyoweza kufanikisha hilo."
Bolt
anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na dhahabu ya mita 200, tukio ambalo
pia alitwaa ushindi wa kwanza katika Olimpiki iliyopita jijini Beijing
mwaka 2008.
Muda
wake wa sekunde 19.19, aliotumia katika mashindano ya ubingwa wa Dunia
mwaka 2009 jijini Berlin, Ujerumani, bado unashikilia rekodi ya dunia ya
kasi.
Alipoulizwa na BBC Radio 5 kama alikuwa akifikiria kushinda mchakato huo wa juzi, Bolt huku akitabasamu alisema:
“Hasa,
ilikuwa katika mawazo yangu kwa miaka kadhaa sasa na ukifuatilia
nilichofanya msimu huu, utaona namna nilivyokuwa najiamini zaidi.
"Sitaki
kusema naweza kufanya hivyo na kisha nikashindwa kufanya hivyo. Lakini
inabaki mawazoni mwangu tu kuwa nataka kufanya hivyo, ndivyo ilivyokuwa
pia."
"Kuna watu wengi walisema siwezi kushinda hapa," alisema Bolt.
"Kulikuwa
na mengi pia yalisemwa. Ni hisia za aina yake kuona nimeyashinda yote
hayo na kuuonesha ulimwengu kuwa bado mimi ni namba moja nab ado mimi ni
bora."
Bolt
atakuwa sehemu ya wakali watakaonza mbio za mita 200 kwenye Uwanja wa
Olimpiki jijini London leo huku fainali ikitarajiwa kufanyika hapo
Alhamisi.
No comments