Wazazi watakiwa kuwa makini malezi ya watoto
Mdhibiti Mkuu Ubora wa shule wilayani Kibaha mkoani Pwani, Revina Lemomo (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Innovate iliyopo wilayani humo, George Ndaki (kulia) na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Munira Seleman
WAZAZI na walezi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani wametakiwa kuendeleza umakini katika malezi ya watoto, kutokana na mmomonyoko mkubwa wa kimaadili.
Rai hiyo imetolewa na Revina Lemomo Mdhibiti Mkuu Ubora wa shule wilayani hapa, kwenye Mahafali ya pili ya shule ya Awali na Msingi ya Innovate iliyopo Kitongoji cha Kibwende, Kata ya Mlandizi wilayani hapa.
Lemomo akiwamwakilisha Mgombe Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini mkoani hapa Hamoud Jumaa, alisema kuwa hivi sasa hali imekuwa mbaya kutokana na kushamili kwa vitendo visivyo vya kiungwana.
"Niwaombe wazazi wenzangu tuwe makini katika malezi ya watoto wetu kwani matukio ya kidhalilishaji yanazidi kushamiri kila kukicha katika majumba yetu," alisema Lemomo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo George Ndaki alisema kuwa, shule inazidi kupiga hatua ya kimaendeleo katika ufundishaji, huku akiongeza kwamba katika mitihani ya Kata imekuwa na matokeo mzuri.
Aliongeza kwamba "Nawapongeza walimu wangu wakiongozwa na Mkuu wao Said Chande, wanaendelea kufanyakazi iliyotukuka kiasi cha kuzidi kupokea wamafunzi kutoka shule mbalimbali," alisema Ndaki.
Taarifa ya wahitimu ikisomwa na wanafunzi Larissa Bunyesi na Joshua Shengoma imeelezea mafanikio ya shule, huku ikigusia changamoto ya kukosekana kwa umeme na ubovu wa barabara.
"Palipo na mafanikio hapakosi changamoto, shule yetu inakabiliwa na ubovu wa miundombinu ya barabara, umeme sanjali na jengo la Utawala lenye Ofisi ya Meneja, Mkurugenzi na Ofisi ya Mwalimu Mkuu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Na Omary Mngindo, Kibwende

"Tunaendelea na maboresho ya miundombinu itayowezesha kuendelea kufanya vizuri katika upatikanaji wa elimu bora zaidi, tunawashukuru wazazi kwa kutuamini," alisema Ndaki.

No comments