Header Ads

ad

Breaking News

Kwaga amshukuru Samia ujenzi Uwanja wa Msoga

Na Omary Mngindo, Kiwangwa

MGOMBEA Udiwani Kata ya Kiwangwa Halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani Malota Kwaga, amemshukuru mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu kwa ahadi ya ujenzi uwanja wa michezo Kijiji cha Msoga.

Aidha, Kwaga alimpongeza Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambae ndio mhasisi wa uwanja huo pasipokumsahau Mbunge Ridhiwani Kikwete, Diwani Hassan Mwinyikondo na wanaMsoga kwa ujumla.

Alitoa pongezi hizo akizungumza na Waandishi wa Habari Kiwangwa, baada ya ahadi hiyo iliyotolewa na Mgombea huyo, alipokuwa kijijini hapo kwenye Kampeni hivi karibuni.

"Tunamshukuru Rais Dkt. Samia kwa ahadi Ile, kwetu wanaChalinze tumeipokea kwa moyo mkunjufu kwani tunakwenda kupata uwanja wa michezo ndani ya Halmashauri yetu," alisema Kwaga.

Aliongeza kuwa, "Wana Msoga wakiongozwa na Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Mbunge Ridhiwani Kikwete, Diwani Hassan Mwinyikondo na wananchi waliuibua uwanja huo kisha viongozi kuanza kufuatilia hatua kwa hatua," alisema Mteule huyo.

Alimalizia kwa kusema kuwa ahadi iliyotolewa na mgombea huyo inakwenda kuwaondoa katika kadhia ya kukosekana kwa uwanja, hivyo anaimani kuwa wana Chalinze wanakwenda kushuhudia Ligi mbalimbali.

"Ahadi ya kiongozi wetu inakwenda kutuletea Ligi mbalimbali zilizochini ya Shirikishi linalosimamia Mpira wa Miguu Nchini TFF, hivyo itakuwa hamasa kubwa nasi kuwa na timu," alimalizia Kwaga.

No comments