Header Ads

ad

Breaking News

BALOZI NCHIMBI:HAKUNA WA KUWAZUIA DKT.SAMIA NA DK.MWINYI KUBAKI IKULU

Na Mwandishi Wetu, Unguja

MGOMBEA Mwenza wa urais wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi hakuna wa kuwazuia Oktoba 29, 2025 kuendelea kusalia Ikulu.

Dkt.Nchimbi amesema kwamba viongozi hao, kwa ushirikiano wao katika kupindi cha miaka mitano wametuliza mfumo wa bei, wameifungua Tanzania na Zanzibar kiuchumi na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza leo Oktoba 8,2025 katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Mkoa wa Kusini Unguja katika Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar, Dkt. Nchimbi amesema mkoa huo ndio amezaliwa Rais Dkt. Samia pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama hivyo wanapaswa kuongoza kwa idadi ya kura wakisema, 'mtu kwao.'

Dkt. Nchimbi amesema jambo kubwa ambalo Rais Samia na Dk.Mwinyi wamelifanya katika miaka mitano waliyoaminiwa na Watanzania na Wazanzibar ni kuilinda imani kwa kutekeleza ilani ya CCM.

"Kazi ambayo wameifanya, inawafanya wana CCM na Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kwenda kupiga kura kwa wingi kwani hakuna wa kuwazuia.

“Katika miaka mitano, viongozi wetu hawa wamesimamia usalama wa nchi yetu, hakuna mpaka uliotikisika, hakuna kipande hata kimoja cha nchi yetu kilichochukuliwa. Usalama, amani na mshikamano, Watanzania bila kudhani dini zao, rangi zao, makabila yao ama Utanzania na Uzanzibar."

Pia, amesema mfumko wa bei wa Tanzania na Zanzibar wameuimarisha na Rais Mwinyi ameahidi ujenzi wa ghala la kuhifadhi chakula ili hali inapobadilika chakula kiwepo na bei isipande na kuwaathiri eananchi.

“Wakati wa ugonjwa wa Korona mwaka 2021, utalii ulishuka lakini viongozi hao wawili waliutangaza upya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour na matunda yake kila mmoja anayaona.”

Mgombea mwenza wa urais Dkt.Nchimbi amesema Dkt.Mwinyi ameahidi akipewa tena ridhaa, anakwenda kutoa ajira 350,000:"Lakini Mwinyi kaniambia hizi ni ajira zimeandikwa kwenye Ilani ila anakwenda kuziongeza."

Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi na msafara wake wamepata nafasi ya kuzuru kaburi la Dk.Muhammed Seif Khatibu, lililopo nyumbani kwake, Kijiji cha Umbuji, mkoa wa Kusini Unguja. Dk Khatibu alifariki dunia Februari 15, 2021.

Awali, uwakilishi wa Chwaka, Issa Gavu Ussi amesema anawakumbusha wanachama, wananchi na watu wote kwamba chama hicho kimepewa kazi."Sisi wana CCM tusichokozeke, wakitusema, wakituchokoza tusichokozeke kwani sisi tuna jukumu la kulinda amani.”

Gavu ambaye pia ni Katibu wa Oganizesheni wa CCM amesema ukiona chama kinazingumza vioja hao wameishiwa hoja huku akisisitiza wapinzani wao hawana hoja za kumsema Rais Samia, hawana hoja za kumsimanga Dkt. Mwinyi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa amesema, Dkt. Nchimbi atakuwa msaidizi mzuri wa Rais Samia huku Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akieleza kwa mshikamano na umoja wetu, CCM inastahili kubaki madarakani, kwa uchumi wa bluee, CCM inastahili kubaki madarakani."











No comments