Header Ads

ad

Breaking News

Hamasa ya Dkt. Samia yazibeba klabu zetu - Jumaa

Na Omary Mngindo, Mlandizi

MTEULE wa Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, Hamoud Abuu Jumaa, amesema kuwa, hamasa ya mwanamichezo namba moja Dkt. Samia Suluhu imeozipeleka klabu nne hatua ya makundi.

Hamasa hiyo ya kutoa kitita cha Shilingi milioni tano kwa kila goli linalofungwa kwenye michuano ya kimataifa maarufu goli la Mama, kwa kiasi kikubwa imechangia kufanya vizuri kwa vilabu hivyo.

"Tumeshuhudia Simba ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Nsingizin Hotspurs ya Uswatini ilipocheza ugenini michuano ya Klabu Bingwa Afrika, jana ikapata suluhu ya pasipokufungana hivyo kusonga mbele hatua ya makundi," alisema Jumaa.

Aliongeza kuwa klabu ya Yanga nayo baada ya kupoteza ugenini Malawi dhidi ya Silver Strikers kwa bao 1-0 nchini Malawi, imekuja kupata ushindi mkubwa wa mabao 2-0 kwenye dimba la Benjamen Mkapa jijini Dar es Salaam hivyo kusonga hatua ya makundi makundi.

"Matukio yote hayo yakiwemo ya Azam FC na Singida Black Star yamechangiwa kwa asilimia 100 na hamasa ya goli la Mama Samia, niwaombe waTanzania tuienzi tunu hii kwani kipindi chake tunafanya vizuri katika michuano ya Kimataifa," alisema Jumaa.

Alisema kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa mwenye bahati kubwa kwani katika kipindi chake cha miaka minne Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa katika medani ya michezo, kwa vilabu vya Mpira wa Miguu pamoja na michezo mbalimbali.

"Watanzania tumetunukiwa tunu hii kubwa, kwani tangu aingie Madarakani kushika nafasi ya mtangulizi wake Hayati John Magufuli tumekuwa tukifanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kimataifa," alimalizia Jumaa.

No comments