Header Ads

ad

Breaking News

DP World yaongeza mapato kutoka trilioni 18 mpaka 32 - Jumaa

Na Omary Mngindo, Mlandizi

KAMPUNI ya DP World iliyokabidhiwa kazi ya kukusanya mapato katika Bandari ya Dar es Salaam, imefanikiwa kuongeza makusanyo ya Serikali kutoka tilioni 18 mpaka 32.

Kampuni hiyo ambayo iliingia makubalino na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu, katika kipindi kifupi kilichopita imeweza kuongeza makusanyo hayo, hatua inayoleta faida kubwa katika nchi.

Hayo yameelezwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Hamoud Jumaa, akizungumza katika mikutano ya Kampeni kwenye Kata mbalimbali Jimboni hapa, ambapo alisema hatua hiyo imetokana na uthubutu wa Dkt. Samia.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na umahiri na uthubutu wa Rais Dkt. Samia Suluhu, akishirikiana na wasaidizi wake sanjali na viongozi mbalimbali aliyefanikisha kuiondoa Kampuni iliyokuwa inakusanya mapato kwenye Bandari hiyo.

"Rais Dkt. Samia Suluhu ambae ndio mgombea wetu wa nafasi hiyo ni mjasiri sana, akisaidiana na washauri pamoja na wasaidizi wake alichukua maamuzi magumu ya kuiondoa Kampuni ya miaka mingi iliyokuwa inakusaanya mapto katika Bandari yetu," alisema Jumaa.

Aliongeza kuwa hatua hiyo imesaidia kuongezeka kwa mapato ambayo yanaendelea kutumika katika Utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika kila sekta, hivyo amewaomba waTanzania kuendelea kuiamini Serikali anayoiongoza.

"Huyu ndio Dkt. Samia Suluhu mwanaMama jasiri ambae alisimama imara kuhakikisha anawatumikia waTanzaia katika nyanja mbalimbali, hivi sasa mapato yameongezeka katika Bandari y, kutoka tilioni 18, sasa tunakusanya tilioni 32," alisema Mgombea huyo.

No comments