Header Ads

ad

Breaking News

Diplomasia ya afya yazidi kuzing’arisha Tanzania na Comoro, kambi ya kibingwa kuzinduliwa leo

Na Mwandishi Wetu

VISIWAa vya Anjouan, Comoro vimeendelea kushuhudia mshikamano wa kidugu kati ya Tanzania na Comoro kupitia ujio wa madaktari bingwa wa Kitanzania kwa ajili ya kambi ya matibabu ya kibingwa.

Jana, msafara wa kwanza wa madaktari bingwa kutoka Tanzania ulipokelewa rasmi na Gavana wa kisiwa cha Anjouan, Dkt. Youssef Zaidou, katika ofisi yake iliyopo jengo la DAR-NADJAH.

Baada ya mapokezi hayo, madaktari walielekea Hospitali za Bambao, Hombo na Pomon ambako wanatarajiwa kutoa huduma kwa kipindi cha wiki moja, kuanzia tarehe 4 hadi 11 Oktoba 2025.

Leo, mapokezi ya msafara wa pili wa madaktari bingwa kutoka Tanzania yamefanyika hapa Anjouan yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakubu, pamoja, mwakilishi wa Gavana, Dkt. Samir Mohamed. Katika mapokezi haya, pia walihudhuria viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro.
Msafara huu wa pili umeongozwa na Mwenyekiti wa Tiba Utalii Taifa, Dkt. Peter Kisenge, akifuatana na Mratibu wa Tiba Utalii kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Asha Mahita na Mwakilisha wa Umoja wa Mataifa (UN) James Tsok Bot.

Jumla ya madaktari 23 wamewasili leo, na kufanya idadi ya jumla ya wataalamu kufikia 49. Hawa ni pamoja na madaktari bingwa, bobezi, wauguzi, wafamasia kutoka taasisi kuu za Tanzania ikiwemo MNH, JKCI, ORCI, MSD na MOI na waratibu wa kambi hiyo maalumu Global Medicare

Madaktari hawa watafanya kazi sambamba na wenzao wa Comoro kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa, kushirikiana uzoefu, na kuimarisha uwezo wa timu za kitabibu za ndani ya Comoro. Ushirikiano huo pia ni sehemu ya kudumisha diplomasia ya kimatibabu na mshikamano wa kidugu na kikanda kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Gavana wa Anjouan alisisitiza kuwa ujio wa madaktari hawa ni “pumzi mpya kwa hospitali zetu na ishara ya urafiki wa dhati kati ya Comoro na Tanzania.”
Kwa upande wa wafanyakazi wa afya wa Comoro, hatua hii imepokelewa kwa furaha na shauku kubwa, huku wengi wakieleza matumaini ya kubadilishana uzoefu na wenzao wa kibingwa kutoika kwa madaktari wa Kitanzania ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi hata baada ya kumalizika kwa kambi hii.

Kambi hii ya matibabu inadhihirisha sio tu msaada wa kiufundi na kibingwa, bali pia ni mfano wa mshikamano wa kikanda katika sekta ya afya ya umma, hususan katika wakati huu ambapo mifumo ya hospitali ya Comoro wakipambana kuiboresha.




No comments