Idd Azzan achukua fomu ya kuomba ridhaa Jimbo la Kinondoni
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Azzan amesema amewiwa kuwania tena nafasi kwa lengo la kuwatmikia wana Kinondoni, lakini kuendeleza kuchukua fomu kama chama kitamchagua na kumpitisha aweze kuwatumikia wananchi katika jimbo hilo.
"Nimechukuwa fomu ya kuomba ridhaa, kama nitachaguliwa ndani ya chama kuwaongoza wananchi wa jimbo hili, basi nitaongoza kwa kufuata na kutekeleza ilani Chama Cha Mapinduzi,"amesema.
Azzan amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kuanzia 2005 hadi 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukuwa fomu ya kuwania nafasi hiyo Juni 29, 2025 katika ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni na kuahidi kuijaza na kuirudisha mapema.
Kisiasa, Azzan amewahi kuongoza Kata a Magomeni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka 2000 hadi 2005, na baadaye Jimbo la Kinondoni kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
Pamoja na mambo ya siasa, Azzan amewahi kuongoza timu ya soka ya Twiga Sports Club kama Mkurugenzi, Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Meneja wa Klabu ya Simba.
"Nimekuwa kwenye siasa kwa mjuda mrefu sana, tangu nikiwa kijana hadi sasa, nina uzoefu wa uongozi kiasiasa na hata kimichezo, naamini nikipata nafasi hii, nitaitendea haki kama nilivyoifanya miaka iliyopita," amesema.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akielekezwa na Katibu wa CCM KInondoni, Jacob Siay jinsi kitu wakati akijaza fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge KinondoniMbunge wa zamani wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akijaza fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge Jimbo la Kinondoni
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge Jimbo la Kinondoni
No comments