Header Ads

ad

Breaking News

Dkt. Samia ametufanyia makubwa Kibaha-Koka

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mkoa wa Pwani anayemaliza muda wake, Silvestry Koka, tayari amechukua fomu

Na Omary Mngindo, Kibaha

MBUNGE anayemaliza muda wake katika Jimbo la Kibaha Mjini Mkoa wa Pwani, Silvestry Koka, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa sana katika jimbo lake la Kibaha Mjini.

Koka ametoa kauli hiyo baada ya kuchukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi hiyo, alipokabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kibaha, Issack Kalleiya.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo, Koka alimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa ya kutekeleza na kuendelea kuitekeleza katika vipindi vyote vya miaka mitano.

"Tunamshukuru Rais Samia kazi kubwa tunayoiona tangu mwaka 2020 hadi 2025, kwa kiasi kikubwa tumeshuhudia mafanikio yatokanayo na maono yake, kipindi hiki kila kona tunashuhudia maendeleo makubwam yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika," amesema Koka.

"Kwenye mitaa yetu, kata hata Makao Makuu ya Mji wa Kibaha tunashuhudia maendeleo makubwa, tumepata manispaa ya mji wetu, manispaa haikuja bure bali kukidhi vigezo vilivyosukumwa na miradi ya maendeleo," amesema Koka.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2025 akiwa mbunge kwa kipindi hicho, Rais Samia alifanya jitihada za kipekee za kuwapatia fedha zilizowezesha Mji wa Kibaha kutoka halmashauri ya mji na kuwa manispaa.

"Natambua kuchukuwa fomu ni wajibu wa kila mwanachama, na mimi nikiwemo, nimechukuwa kutetea nafasi yangu, natambua kuchukua fomu ni wajibu wa mwanachama na wajibu wangu pia," amesema Koka.

"Ninatambua ni wajibu wa mwanachama yeyote, lakini kuteuliwa ni wajibu wa vikao,  nikiwa mbunge ninayetetea kwa miaka 15, natambua kuteuliwa ni kazi ya vikao," amesema.

Amesema vikao kuanzia ngazi za wilaya hadi kitaifa, ndiyo vyenye wajibu wa kufanya uteuzi, hivyo atakayeteuliwe hata kama hajateuliwa, jukumu lake litakuwa la kumnadi mgombea atayeteuliwa na mkutano mkuu wa taifa jijini Dodoma.

"Nitasimama imara kumtetea mgombea wetu wa urais Dkt. Samia pia mwenza wake Dkt. Emmanuel Nchimbi na mgombea wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, hata nisipoteuliwa nitawajibika kuwanadi na kuwapigania viongozi wetu wote washinde," amesema Koka.

"Kuna msemo niliokuwa nausema kuwa, nimeikuta CCM imara Kibaha au katika Jimbo la Kibaha, nawajibika kuendelea kuifanya iwe imara hata kama nikitoka madarakani nitakuwa kiongozi mstaafu, nawajibika kuiacha ikiwa imara kama nilivyoikuta, nimejiandaa kuhakikisha hilo," amesema Koka.

No comments