Header Ads

ad

Breaking News

Wazazi waipongeza GEL kwa elimu kuhusu fursa za masomo nje ya nchi

Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link Abdulmalik Mollel akiwape elimu wanafunzi wanaotarajiwa kwenda kusoma nje ya nchi jinsi ya kukamilisha taratibu 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

ZAIDI ya wanafunzi 200 wanatarajiwa kusafiri kwenda masomoni kwenye mataifa mbalimbali kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 hivi karibuni kuanza pitia uratibu wa Global Education Link (GEL).

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalick Mollel, wakati wa kikao baina ya wanafunzi hao na wazazi wao kuhusu kukamilisha taratibu za safari.

Wanafunzi hao wanatarajiwa kusafiri kwenda masomoni kwa nchi za Uingereza, Canada, Marekani Malaysia, Poland, Uturuki na India.

Kikao hicho kilifanyika ofisini hapo ambacho kililenga kuwaelimisha wanafunzi hao taratibu na kanuni wanazotakiwa kufuata wanapokuwa masomoni nje ya nchi zikiwemo mila, tamaduni na desturi za nchi wanazotarajia kwenda.

“Ni jukumu la GEL kuhakikisha maandalizi yote ya visa na nyaraka zingine zimekamilika na kuhakikisha wanafunzi ambao wameniamini na wazazi wao kuwaelekeza vizuri na jukumu la mwanafunzi ni kusema kozi anayokwenda kusoma,” amesema

“Mwanafunzi atasema anataka kozi gani anataka kusoma nchi gani na atasema anataka kukaa kwenye chumba cha aina gani na mzazi anatakiwa kujiridhisha na kozi na nchi anayokwenda kusoma,” amesema Mollel.


“Mzazi unatakiwa kuwa makini sana kuchagua nchi ambayo mtoto wako anakwenda kusoma kwasababu lazima uzingatie uwezo wako wa kiuchumi ili usipeleka mtoto wako halafu mambo yakawa magumu huko mbeleni,” ame
sema.

Mollel amesema kikao kama hicho cha wazazi na wanafunzi kimekuwa kikichambua mila na tamaduni ambazo mwanafunzi anapaswa kuzingatia kulingana na nchi anayotarajia kwenda kusoma ili asikutane na vikwazo anapokuwa nchini humo.

Mollel amesema ni muhimu wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kujua kupika wenyewe ili kurahisisha maisha ya kukaa nje ya nchi kwani vyuakula vya kununua wakati mwingine ni gharama kubwa.

“Awe mvulana au msichana anapaswa kujua kupika kwasababu huwezi kuwa unakula hotelini kila siku gharama za maisha zitakuwa juu kwa hiyo kama unaishi na rafiki zao mnapangiana zamu za kupika na maisha yanakuwa nafuu kidogo,” amesema Mollel

Mollel amesema GEL imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa kitaaluma na tabia kwa wanafunzi wote wanaosafiri kupitia taasisi yake ili kuhakikisha wanahitimu wakiwa na alama nzuri.

Alisema mbali na kufuatilia maendeleo ya taaluma, GEL imekuwa ikifuatilia usalama wa wanafunzi hao nje ya nchi na hata ilivyotokea vita baina ya Urusi na Ukraine GEL ilisimama imara na wanafunzi wote waliokuwa Ukraine walirudi salama nchini.

Mollel amesema ni muhimu kwa wazazi nao kufuatilia kwa karibu maendeleo ya tabia na taaluma ya watoto wao kwani wasipofanya hivyo baadhi wanaweza kudanganya na mwisho wa siku wanashindwa kuhitimu masomo yao.

“Mwanafunzi unapaswa kufuata kile kilichokupeleka kule, umeenda kusoma basi wewe kazi yako ni kusoma achana na starehe na mambo yasiyokuwa ya kitaaluma kwasababu mzazi anajinyima vitu vingi ili wewe usome sasa usipohitimu unamtesa sana mzazi,” amesema

Mmoja wa wazazi walioshiriki kikao hicho, Deogratius Uiso alisema amefurahishwa na maelezo yaliyotolewa na GEL kuhusu fursa za masomo kwenye mataifa mbalimbali duniani na mila na tamaduni.

“Sisi wazazi vikao kama hivi vinatusaidia sana kupata mwanga wa mtoto anapokwenda mfano tumeambiwa kuwa anaweza kukutana na changamoto ya mila na tamaduni ambazo anapaswa kuendana nazo ili kuishi vizuri,” a
mesema.

No comments