UMMY MWALIMU ASHIRIKI MIKUTANO YA KATA 3 KWA SIKU KUZISAKA KURA ZA CCM TANGA MJINI
Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu Novemba 25,2024 ameendelea kuwanadi wagombea wa CCM wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jimbo la Tanga Mjini.
Mhe Ummy ameshiriki mikutano ya hadhara katika kata ya Maweni (Mtaa wa Kange), Kata ya Pongwe (Mtaa wa Pongwe kusini) na Kata ya Kirare (Mtaa Mapojoni).
Mkutano wa Kange ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ustadh Rajab Abdurahman ambae ameeleza kuwa kutokana na Kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan, CCM itashinda katika Mitaa, Vijiji na Vitongoji vyote vya Mkoa wa Tanga.
Aidha Mhe Ummy kwa upande wake ameendelea kuwataka wana Tanga Mjini kuchagua wenyeviti wa CCM wa CCM kwa kuwa ndio wenye nguvu na dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo katika mitaa yao chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Tanga Mjini
25/11/2024
No comments