Header Ads

ad

Breaking News

Mwanariadha wa Marekani David Torrence afariki dunia

ARIZONA, Marekani
Mwanariadha wa mbio za masafa ya wastani kutoka Marekani ,David Torrence amepatikana akiwa amefariki katika kidimbwi cha kuogelea katika jimbo la Arizona akiwa na miaka 31.


Torrence alishinda fedha katika mbio za ubingwa wa dunia za kupokezana vijiti mwaka 2014 na alimaliza wa pili pia katika mbio za bara la Amerika mwaka 2015.

Alibadilisha uraia kutoka Marekani hadi Peru na akawakilisha taifa hilo lake jipya katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016.

"Wachunguzi wa jinai wamebaini kwamba hakuna dalili zozote dhahiri kwamba huenda aliuawa," taarifa ya polisi imesema.
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Shirikisho la riadha la Marekani limetuma rambirambi kupitia Twitter

David Torrence alimaliza wa 13 mbio za 5,000m upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016 ambapo Mo Farah alishinda dhahabu.

No comments