Header Ads

ad

Breaking News

MAJINA NANE YAPITISHWA MCHUJO WA AWALI UONGOZI TPLB



Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Waliopitishwa kuwania uenyekiti wa Management Committee ni Clement Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan Crysostoms amepitishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti. 

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.

Edga Chibura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.

Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au marais wa klabu husika.

Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.

Wakati huo huo, timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.

Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba.

Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

 Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu.

 -4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa mpira wa miguu.


No comments