Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia baharini
![]() |
China ni moja ya nchi zinazodai kumiliki maeneo ya kusini mwa bahari ya China. Getty Images |
China ni moja ya nchi zinazodai kumiliki maeneo ya kusini mwa bahari ya China
Marekanai
hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa
bahari ya China, waziri wa ulinzi wa Merekani James Mattis ameonya.
Akiongea katika mkutano wa kiusalama huko Singapore, Bwana Mattis amesema kwamba hatua ya Uchina ya kutengeneza visiwa bandia na kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika bahari ya kimataifa unahatarisha amani katika eneo hilo.
Hata hivyo amesema ugomvi kati ya Marekani na Uchina unaweza kuepukika, na akaipongeza Uchina kwa juhudi zake za kukabiliana na mgogoro unaotokana na uundaji wa zana za kinyuklia nhini Korea Kaskazini.
Baraza hilo liliunga mkono kwa wingi vikwazo hivyo baada ya mazungumzo ya majuma kadha kati ya Marekani na China
No comments